Friday, April 25, 2014

SHTUKA: FAHAMU ZAIDI KUHUSU UTI "YUTIAI"..UGONJWA UNAOWASUMBUA WADADA WENGI HIVI SASA!

 Tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo kitaalamu linaitwa ‘Urinary Track Infections’ au kwa kifupi ‘UTI’ au imezoeleka kama Yutiai.


Watu wengi wanafahamu Yutiai lakini kila mmoja anaielezea kivyake. Ilimradi tu kuna mabadiliko katika njia ya mkojo au ukeni basi mtu anajua ni Yutiai.
Viungo vinavyohusisha mfumo wa mkojo ni figo, mirija ya kusafirisha mkojo toka katika figo hadi kwenye kibofu chenyewe na njia ya kutolea mkojo nje, Yutiai huathiri sehemu hizi tu.  Endapo mwanamke atatokwa na uchafu ukeni hiyo siyo Yutiai.
Muwasho sehemu za siri pia siyo Yutiai. 

Jinsi tatizo linavyotokea
Maambukizi katika njia ya mkojo huanzia kwenye njia ya kutolea mkojo nje kwa mwanaume na mwanamke. Maambukizi haya yana tabia ya kupanda hadi ndani ya kibofu na kuendelea kwenye ‘Ureter’ hadi kwenye figo.
 

Maambukizi yapo aina nyingi, inaweza kuwa maambukizi ya magonjwa ya ngono au uhamisho wa bakteria wa ukeni na wale wa haja kubwa kwenda kwenye njia ya mkojo. 

Uhamisho unatokana pale mwanamke anapojisafisha ukeni au katika njia ya haja kubwa na kusukumia kwa mbele. Kwa kila binadamu, sehemu ya haja kubwa ina bakteria wake ambao hawana madhara huko lakini wakiingia katika njia ya mkojo wanaleta madhara. 

Wapo bakteria wengine ukeni ambao huko hawana madhara ila wakiingia katika njia ya mkojo wanaleta shida. 

Maambukizi pia huweza kusababishwa na uhamisho wa bakteria kutoka sehemu nyingine  kwenda katika njia ya mkojo. Mfano, kujisafisha sehemu za siri kwa kutumia maji yasiyo safi, kutumia chombo kisicho safi au unapojisaidia yale majimaji yanayokurukia sehemu za siri. 

Nani anaweza kupata Yutiai?
Watu wote wanaume na wanawake wapo hatarini kupata ugonjwa huu. Wanaoathirika zaidi ni wanawake, watoto na wazee.


Wanawake na watoto huathirika zaidi kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vya kutolea mkojo na haja kubwa vipo karibu, wazee ni kutokana na kushindwa kujihudumia. 

Wanawake wajawazito pia wapo katika hatari hii kama hawatazingatia usafi wa hali ya juu katika kipindi hiki. 

Wanaume ambao hawajafanyiwa tohara pia wapo katika kundi hili. Wengine ni wanaume wenye tabia ya kulawiti pia husumbuliwa sana na Yutiai na hata kupatwa na tatizo la kuziba kwa njia ya mkojo katika umri wa miaka chini ya 45. Matatizo ya mkojo katika umri zaidi ya miaka 45 hutokana zaidi na hitilafu katika tezi dume. 

Dalili za Yutiai
Mtoto mwenye tatizo hili daima hulialia, hupoteza hamu ya kula na hupatwa na homa za vipindi na hudhoofika.Mwanaume na mwanamke mtu mzima huhisi kuwa mchovu, mkojo kuwa mzito na harufu mbaya na wakati mwingine mkojo huwa na damu. Maumivu chini ya tumbo na huzunguka kiuno na kusambaa miguuni.
 

Huhisi homa au baridi hasa vipindi vya jioni, maumivu husambaa hadi upande wa juu ubavu wa kulia na kushoto, ukikojoa utahisi mkojo wa moto. 

Uchunguzi
Vipimo mbalimbali hufanyika kuangalia athari zinazotokea kutokana na maambukizi.


Kipimo cha kuotesha mkojo ‘Urine Culture and Sensitivity’ ndiyo mahususi kwa ajili ya Yutiai, kipimo hiki majibu yake huchukua zaidi siku mbili na hutumia vifaa maalum kuchukulia mkojo. Kipimo kitaonyesha aina ya bakteria na anakufa kwa dawa gani.
 

ipimo vingine vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa, mfano kipimo cha Ultrasound, vipimo vya damu na vingine. 

Matibabu na ushauri
Tiba hutolewa baada ya majibu ya vipimo. Ni vema kuwa msafi wa maungo na nguo za ndani pamoja na mazingira ya choo.

Kunywa maji mengi kila wakati, kuwa na mkojo wenye rangi iliyokolea siyo dalili ya kuwa na Yutiai.

Wanawake na watoto wadogo wajisafishe kuelekea kwa nyuma, watoto wachanga wasikae na nepi au pambasi zenye mkojo na kinyesi kwa muda mrefu.
Wahi hospitali kwa uchunguzi wa kina.

No comments:

Post a Comment

INAYOFANANA

QWWWWWWWWWWWWWWW

Popular Posts